Mwanza ilianzishwa na Wajerumani wakati wa koloni ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani. Mahali paliteuliwa kutokana na nafasi ya bandari asilia upande wa kusini ya Ziwa Viktoria. Wajerumani waliuita mji kwa jina "Muansa" inaaminiwa ilikuwa matamshi yao ya neno "nyanza". Walijenga boma kubwa iliyoendelea kitovu cha mji. Takwimu ya Kijerumani ya 1912 ilihesabu wazungu 85, Wagoa 15, Wahindi wengine 300 na Waarabu 70 lakini haikutaja wakazi Waafrika. Palikuwa na makampuni ya biashara 12 ya kizungu na 50 ya Wahindi.
Mkoa wa Mwanza ni kati ya mikoa 31 ya Tanzania wenye postikodi namba 33000[1]. Umepakana na Geita upande wa magharibi, Shinyangana Simiu upande wa kusini na Mara upande wa mashariki. Ziwa la Viktoria Nyanza liko kaskazini.
Wilaya
Kabla ya kumegwa na kuzaa mkoa mpya wa Geita, mkoa wa Mwanza ulikuwa na wakazi 2,942,148 (sensa ya mwaka 2002) katika wilaya 8 ukiwa na eneo la 19,592 km2. Wilaya ndizo Ukerewe, Magu, Sengerema, Geita, Misungwi, Kwimba, Nyamaganga na Ilemela. Jiji la Mwanza lina ndani yake wilaya za Nyamagana na Ilemela.
Ramani | Wilaya au manisipaa | Wakazi (2002) | Tarafa | Kata | Kijiji | Eneo km² |
---|---|---|---|---|---|---|
Wilaya ya Geita | 712,195 | |||||
Wilaya ya Ilemela | 265,911 | |||||
Wilaya ya Kwimba | 316,180 | |||||
Wilaya ya Magu | 416,113 | |||||
Wilaya ya Misungwi | 257,155 | |||||
Wilaya ya Nyamagana | 210,735 | |||||
Wilaya ya Sengerema | 501,915 | |||||
Wilaya ya Ukerewe | 261,944 | |||||
Jumla | 2,942,148 | 19,592 | ||||
Mkoa wa Mwanza una Halmashauri za Wilaya tatu sita ambazo ni Geita, Sengerema, Magu, Misungwi, Kwimba na Ukerewe na Halmashauri ya Jiji la Mwanza inayohudumia wilaya za Nyamagana na Ilemela. |
Wakazi[hariri | hariri chanzo]
Majimbo ya bunge
Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi yafuatayo:
- Buchosa : mbunge ni Dk. Charles Tizeba (CCM)
- Ilemela : mbunge ni Angelina Mabula (CCM)
- Kwimba : mbunge ni Mansoor Hirani (CCM)
- Magu : mbunge ni Kiswaga Boniventura (CCM)
- Misungwi : mbunge ni Charles Kitwanga (CCM)
- Nyamagana : mbunge ni Stanslaus Mabula (CCM)
- Sengerema : mbunge ni William Ngeleja (CCM)
- Sumve : mbunge ni Richard Mganga Ndassa (CCM)
- Ukerewe : mbunge ni Joseph Mkundi (Chadema)
0 comments:
Post a Comment